Friday, March 24, 2017

Faida za Ulaji wa Bamia Kiafya

Bamia ni zao ambalo lina faida lukuki katika ulimwengu wa kibiashara. Wapo wakulima mbalimbali ambao wamekuwa wakinufaika na zao hilo.

lakini ukitazama katika sura nyingine bamia zina faida nyingi sana kiafaya hasa pale mtu ambapo anapozitumia, na faida hizo husaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza na kutibu maradhi mbalimbali.

Na Kwa mujibu wa mtandao wa healthandcure.com uliwahi kuwanukuu baadhi ya wataalam wa afya wakieleza kwamba watu wanaosumbuliwa na maradhi ya:

1. mfumo wa chakula kama vile vidonda vya tumbo na mengine yanayofana na hayo wanaweza kupata ahuweni au kupona kabisa ikiwa watakula bamia.

2.Aidha, faida nyingine zinazotokana na ulaji wa bamia ni pamoja na kuwa chanzo kizuri cha vitamin A,

3. Ulaji wa bamia husaidia kuboresha uwezo wa macho kuona vizuri.

4. Vilevile bamia inasaidia kuweka vizuri  kiwango cha sukari mwilini.

5. Mbali na hayo, bamia pia husaidia kulainisha choo.

6. Bamia husaidia sana kwa mtu mwenye matatizo ya kula.

7. bamia huimarisha mifupa, huongeza kinga dhidi ya magonjwa ya figo, saratani pamoja na pumu.

Hayo ni baadhi ya maajabu ya magonjwa ambayo yanawezwa kutibiwa na ulaji wa bamia, hivyo ni vyema ukatumia bamia mara kwa mara kwa kuimarisha afya yako.

Monday, March 13, 2017

Tangawizi Nayo Dawa!!!!.Soma hapa.

Vitamin B6 iligunduliwa mwaka 1934 na Dr. Paul Gyorgy huko Hungary na akabainisha wazi kuwa ml.100 za B6 ni dozi tosha kwa siku kwa wagonjwa wenye umri wa miaka 19 hadi 70 katika kupambana na kichefuchefu na hata kuzuia kutapika pia.

Tangawizi licha ya kuwa na uwezo wa kumaliza tatizo hili, bado imegundulika kuwa na uwezo tena wa kukinga maradhi ya uvimbe ndani ya mwili wa binadamu ambao husababisha wengi kupatwa na maradhi ya saratani za aina tofauti tokana na uvimbe huo.

Hata hivyo, ukiwa unatumia tangawizi katika kila mlo wako kwa muda mfupi tu utajikuta maumivu ya mgongo, kiuno, maungio ya miguu na mikono yamepungua na kama siyo kuisha kabisa. Hii ndiyo kazi halisi ya tangawizi duniani na leo ni fursa kwako kulijua hili.

Kichefuchefu ni ugonjwa unaowasumbua watu wengi duniani na chanzo kikiwa ni kupanda kwa joto la mwili kunakosababishwa na homa au maambukizi ya bakteria wa maradhi tofauti yakiwemo malaria pia.


 Hata hivyo, ugonjwa huu huwakumba sana akina mama wajawazito na kujikuta wakitapika mara kwa mara na kupoteza maji na madini mengi mwilini na kuhatarisha maisha yao wenyewe, watoto waliomo matumboni na pengine kuhatarisha maisha yao wote mama na mtoto.

Mbali na akina mama wajawazito kuugua ugonjwa huu watu wengine ambao hukumbwa na ugonjwa ni wasafiri wa baharini, wagonjwa wanaotumia dawa kali, watumiaji wa mihadarati, walaji wa vyakula vyenye sumu baridi, walevi wa kupindukia na pengine hata wanaokutana na harufu mbaya na kali kushinda uwezo wa kuimudu pia hupatwa na kichefuchefu na mwisho ni kutapika.

Ukiachana na sababu hizo, bado pia wagonjwa wa kidole tumbo yaani ‘appendix/appendiatis’ au hata wanaougua magonjwa ya mchafuko wa tumbo kama kuharisha na kipindupindu pia hupatwa na kichefuchefu na hutapika sana wanapokosa msaada wa tiba.

Kwa maradhi haya, kitu cha haraka kukifanya ni kunywa maji mengi huku ukijikongoja umwone
daktari haraka kwa kuwa aina nyingi za maradhi haya huua haraka sana kwa kukosa maji na madini muhimu mwilini kwa kutapika.

Ila, ulimwengu wa kisasa umetuletea teknolojia sahihi zinazokubalika duniani kote kwa kutengeneza vyakula lishe ambavyo ni mkandamizo wa vitamini, madini na tindikali muhimu kwa afya. Vyakula hivi vyenye kanuni ya vidongelishe na ungalishe vipo vya aina nyingi tu madukani na vinasaidia watu kupona maradhi mbalimbali bila kwenda hospitali.

Kama hujatumia tangawizi kwa muda mrefu na unajihisi kuwa na kichefuchefu mara kwa mara basi unaweza kuanza kutumia mara moja japo hutaona matokeo haraka ila ukitumia dawalishe ya B6 basi utapata nafuu haraka sana.

Akina mama wajawazito wao wanashauriwa kutumia dawalishe yao maalum iitwayo ‘Pregnancy Shake’ na MOM2B ya vidonge ambayo pamoja na vitamins nyingi zilizomo humo pia kuna vitamin B6 ambayo itamfanya ajisikie mwenye afya njema siku zote atakazobeba mimba yake huku akijihakikishia kujifungua salama.

Kama wewe huna maradhi yoyote ila ungependa kujiwekea kinga ya kutosha kwa maradhi basi unashauriwa utumie Dawalishe za B6 au uanze mara moja kuihusisha tangawizi katika milo yako yote ya kutwa nzima na hakika utaonekana ukitabasamu muda wote kwa kuwa utakuwa na kinga ya
maradhi, hutaumwa viungo na hutasikia kichefuchefu tena katika maisha yako.

Ukiona mtu anatapika, basi chemsha maji yenye tangawizi yapooze na umpe anywe na kutapika kutaisha huku ukimuwahisha kwa daktari kwa msaada zaidi.

Mazoezi Kudhibiti Ugonjwa Wa Kisukari.

Kila mara tunashauriwa kuweza kufanya mazoezi kwa sababu mazoezi yana faida sana katika kuimarisha afya zetu, kuimarika kwa afya pekee yake haitoshi bali mazoezi ya mwili yanasaidia kwa kiwango kikubwa kuzuia magonjwa mengi sana.

Lakini kwa leo naomba tuangazie hasa umuhimu wa kufanya mazoezi kwa mtu mwenye kisukari, kwani kufanya mazoezi kwa mtu ambaye anaishi na ugonjwa wa kisukari kuna faida zifuatazo:

1. Mazoezi yanasaidia katika kudhibiti kiwango cha sukari katika mwili.

2. Yanasaidia kupunguza uzito wa mwili.

3. Mazoezi yanasaidia kudhibiti shinikizo la damu kwa kiwango kikubwa sana.

4 pia mazoezi yanasaidia kuweka kiwango cha mafuta kuweza kukaa katika hali nzuri.

5. Mazoezi ya mwili yanasaidia kupunguza msongo wa mawazo kwa kiwango cha hali ya juu sana, hii endapo utaamua kufanya kazi ushauri huu.

Baada ya kuona faida za kufanya mazoezi ya mwili, pia wataalamu mbalimbali wa afya, wanazidi kutuhimiza ya kwamba, mtu anatakiwa kutenga angalau nusu saa kwa ajili ya kufanya mazoezi kwa kila siku.

Hivyo zingatia yafuatayo  katika kufanya mazoezi:
Kama hujafanya mazoezi kwa muda mrefu, anza na mazoezi madogo madogo na kuongeza viwango taratibu vya baadhi ya mazoezi kila siku.

Pia mazoezi haya Unaweza kujiunga na gym, sehemu ambayo utapata mtaalamu wa kutoa mazoezi kwa watu wenye matatizo mbalimbali. Kupata mtu wa kukusaidia na kukuelekeza katika mazoezi kutakupa ari ya kufanya mazoezi kwa umakini zaidi. Isitoshe, gym zina vifaa vya kisasa vya kukupa vipimo vya mazoezi yako na maendeleo yako.

Kama huna uwezo wa kwenda gym wala usipate tabu, fanya mazoezi ambayo unayafahamu ambayo yatakufanya utoke jasho.  

Wednesday, March 8, 2017

Kwanini uache kutumiasukari

Sababu zitakazokufanya uache kutumia sukari.


Sukari ni moja ya viungo vinavyyopendwa na kutumika sana dunia nzima, sukari inaweza kupatikana kiasilia mfano kwenye maziwa, matunda, asali, miwa, wali na kadhalika na nyingine ni  ile ambayo inatengenezwa kiwandani ili iweze kuungwa kwenye vyakula na vivywaji kama soda, biskuti, chocolate, chai, maandazi, keki, ice cream, pipi na kadhalika.

aina hii ya sukari ambayo inapatikana kwa kutengenezwa kiwandani ni hatari sana na moja ya vyanzo vikuu vya vifo duniani..

kuna aina tatu muhimu za sukari ambazo ni
glucose; hii ni sukari ambayo inatengenezwa na viumbe hai vyote vilivyoko duniani na hutupa nguvu kwa wingi lakini pia hutengenezwa viwandani.

sucrose; hii ni sukari kutoka kwenye mimea kama mahindi, ngano, miwa, uwele na kadhalika inatengenezwa na mimea lakini pia huweza kutengenezwa kiwandani au maabara.

fructose; hii ni sukari inayopatikana kwenye matunda, ni moja ya sukari hatari sana ikiliwa kwa kiasi kikubwa. kwa hali ya kawaida mtu hawezi kula matunda mpaka ikazidi mwilini lakini anaweza kula iliyotengenezwa kiwandani mpaka ikazidi mwilini.sukari tunayotumia majumbani ni mchanganyiko wa glucose na fructose.

watu wengi wamekua wakililia sukari pale inapokosekana au kupanda bei lakini naomba nikwambie kwamba kulilia sukari ni kulilia kifo kwani madhara yake yanatisha...hebu tuone hasara za sukari ile inayotengenezwa kiwandani au kuungwa kwenye vyakula...

inaharibu meno; sukari haina virutubisho au vitamini zozote, ukila sukari haupati faida yeyote kwenye mwili zaidi ya nguvu ambazo unaweza kuzipata kwenye vyakula vingine, lakini pia sukari hutengeneza mazingira mazuri mdomoni kwa bacteria kuweza kushambulia meno na kuyaharibu hivyo walaji wa kubwa wa pipi, biskuti, soda na kadhalika meno yao hutoboka sana.

ugonjwa wa maini; ugonjwa huu kitaalamu kwa jina la non alcoholic fatty liver disease unasababishwa na ulaji mwingi wa sukari ya aina ya fructuse ambayo hubadilishwa na mwili na kua mafuta...mafuta hayo hujazana kwenye maini na kusababisha magonjwa mengine ya maini kama saratani na kushindwa kazi kwa maini.

kushindwa kuacha au addiction; sukari ikitumika muda mrefu husababisha ubongo kumwaga homoni nyingi kwa jina la dopamine, homoni hii humfanya mtu azoee na kushimdwa kabisa kuacha matumizi ya aina fulani ya sukari..mfano kuna watu hawawezi kumaliza siku bila kunywa aina fulani ya soda kwani hawawezi kuvumilia ile kiu.

unene na vitambi; kama tulivyosema hapo mwanzo, sukari ikishaliwa, hubadilishwa na mwili kua mafuta na kuhifadhiwa mwilini...mwili unahifadhi sana mafuta tumboni na makalioni, mafuta haya ni hatari sana kwa afya ya mwili kiujumla..kama unataka kupunguza uzito leo, kitu cha kwanza ni kuacha kutumia sukari zote.

humfanya mtu ale sana chakula; tafiti moja zilifanyika zikagundua kwamba ulaji wa sukari ya aina ya fructose ni tofauti na ulaji wa glucose...ulaji wa vyakula vilivyoongezewa sukari ya fructose humfanya mtu asiridhike na chakula alichokula na hivyo atahitaji kula zaidi na zaidi...hii husababishwa na kuzuiliwa kwa homoni kitaalamu kwa jina la heptin, homoni huu hufanya kazi ya kutoa taarifa kwenye ubongo pale mtu anapokua ameshiba ili asiendelee kula, kushindwa kazi kwa homoni hii husababisha mtu ale sana kupitiliza...kama ni soda atakunywa nyingi zaidi, kama ni chakula atakula kingi zaidi, kama ni ice cream atakula nyingi zaidi na kadhalika...

saratani mbalimbali; tafiti zilizofanyika zimeonyesha kwamba kuna mahusiano makubwa sana kati ya kula sukari na kupata kansa...kwanza sukari husababisha homoni aina ya insulini ambayo inatumika kuvunja sukari kua juu sana muda wote na kusabababisha kansa lakini pia sukari huumiza baadhi ya mifumo ya mwili na kuleta kansa.

magonjwa ya moyo; kwa miaka mingi watu wamekua wakilaumu ulaji wa nyama nyekundu kua chanzo kikuu cha magonjwa ya moyo kwa kutengeneza aina fulani ya mafuta kitaalamu kama very low density lipoprotein ambayo huziba mishipa ya moyo..sukari aina ya fructose imegundulika  ikilika nyingi husababisha kuongezeka sana kwa mafuta haya na ni hatari sana kuliko nyama.

ugonjwa wa kisukari; ulaji wa sukari nyingi husababisha homone insulini ambayo ianahusika kuingiza sukari ndani ya seli ili tupate nguvu kushindwa kufanya kazi..hii husababisha kuwepo kiwango kikubwa sana cha sukari kwenye damu ambacho hupelekea kuanza kwa ugonjwa wa kisukari..ugonjwa huu huleta madhara makubwa kama upofu, kiharusi, na kushindwa kufanya kazi kwa moyo.

ugonjwa wa chunusi; utafiti uliofanyika mwaka 2008 uligundua kwamba ulaji wa sukari husababisha kuongezeka kwa ugonjwa wa ngozi wa chunusi sababu ya mafuta yanayopatikana sukari inapohifadhiwa mwilini..mafuta haya husiba matundu ya ngozi na kuleta chunusi.

hatari ya fangasi za mwili;
hatari ya fangasi mwilini; uwepo wa sukari nyingi mwilini husaidia fangasi kushambulia na kugawanyika haraka sana mwilini.

mwisho; mbadala mzuri wa sukari ni asali, asali ina sukari ambayo inapatikana kiasilia bila kupita mikononi mwa binadamu...lakini pia ina uwezo wa kuharibu kemikali na sumu kali za mwili ambazo zinaleta kansa..ni vizuri kuanza kutumia asali kwenye chai yako badala ya sukari lakini pia kuachana na ulaji wa sukari ambazo hazina faida mwilini mwako ambzo huongezwa kwenye vyakula mfano maandazi, keki, soda, biskuti, chocolate na vitamu vyote unavyovihamu.